Advertisement


Nyasubi ndani ya mbanyu Kiri, wamemchokoza Bea

Kwako ndugu hii ni barua ya wazi Barua yenye mambo kadhaa sio ya kuomba kazi Salamu habari za mda huu  Husika ana kichwa cha habari hapo juu

Mi nilifunzwa kusimama pale napokwenda chini Nilifunzwa kuacha kazi pale pindi pale anapoadhini Huu uandishi zaidi ya Ngug’i wa Thiong’o Share Bandra bahati ya uandishi wa Sigongo

Nami nasikia sina uhakika kuhusu uzembe Jibu kubakia simba alafu kuikataa mazembe Vilabu ni taasisi nembo zalisha pesa Ubaya wa kumtegemea mwarabu akinuna anaposti Twitter

Waliloweka miguu wasisinzie wakariri sana Michoro ya test-tube na bunsen burner Elimu ni kupanua akili mawazo chanya Wanachofeli ni kutegemea kusoma waje kufanya

Kila kitu ni fursa hii nchi ina vituko Mwenye mvi alitemwa huko leo kapokewa hukoo Kumkumbatia anayekufilisi  Ni sawa na kuozesha mgumba kwa kasisi

Na hii barua sio kitabu cha Wayahudi Torati ya Musa au Zaburi ya Daudi Msilie masista duu wabishi mliokataa umama ntilie Leo una mpa heshima Shishi

Ka mlihisi ni dhawabu, mnajidanganya sasa Pesa ya kamari kuchangia ujenzi wa madarasa Barua hii bado ina kurasa nyingi Endelea kusoma ndani utajifunza vingi

Ah-ah naomba msiniite mi nabii Ambaye nimeshushwa kwa ukoo wa kizazi hiki Ah-ah mi nimeandika tu barua Na sina maana kama nafaa kuitwa Masii

Chonde naomba msiniite mi nabii Sikuwa na lengo baya kuandika barua hii La hasha sitaki kutukuzwa  Mwenye akili atasoma na mpuuzi atapuuza

Na bongo kazi kubwa ni ile ya kutafuta kazi That’s why niliweka nguvu kwenye kilimo na ufugaji Mtachachawa si mlitaka sifa Mlimeza vega power kwa lengo la kutibu kichwa

Dodoma mmh mmh kelele paka taabu Kurushiana vijembe kama band za taarabu Barua hii haina kusudi baya  Ina lengo la kujenga umoja sio kujigawa

Hii ni vita ya madaraja zaidi ya kibaka na afande Huku EF apande kule Dodoma apande Ni shirikisho team zetu ni vimeo Ati kuingia kwenye kashfa ya kupanga matokeo


Advertisement


Hatuamini kwenye kufanikiwa wote Mmoja afanikiwe mwingine fitna atoke Hii ndio Bongo, ndio maana wanacheka mnapo Nipeleka nikasomee udoctor veta 

Ankali maziwa wananywea mseto Umeshika darubini unataka kuiona pepo Shughuli ni pevu hayawi uliyotabiri Inabidi kuwe kwa kati kunoti albadiri

Au wana laana si katembea na bibi Yaani ashura si kwa christmas si anakula Idi Kutumia zaidi ya kile nachopata Ni sawa na papi kuwa kiongozi wa bakwata

Eeh kakosea masharti ndio maana napagawa Badala ya kuzioga gonjwa zikazinywa dawa Tunzeni hii barua vizazi vitaisoma Mtajiskia vibaya mkisoma mkachoma

Ah-ah naomba msiniite mi nabii Ambaye nimeshushwa kwa ukoo wa kizazi hiki Ah-ah mi nimeandika tu barua Na sina maana kama nafaa kuitwa Masii

Chonde naomba msiniite mi nabii Sikuwa na lengo baya kuandika barua hii La hasha sitaki kutukuzwa  Mwenye akili atasoma na mpuuzi atapuuza

Nacha halii mesri mitaani hadi utamchoka Nyihogo kwa mama njunju mwananyamala kwa kopa Mi ni mpole mkinichukiza nawalaza hoi Nawarushia makonde Nyasubi wananiita Konde Boy

Ondoa shaka, Nacha Dr Mwaka Hii ni la TZ la dhamani kwa Kenyatta Mlizoea kubebwa da leo bungi liko na gwanda Fubegu itavunjika nyonga naacha winger toka danda

Nikifa nitakumbukwa Kasurwa hadi kibondo Naacha pengo na historia zaidi ya Mbozi na Kibondo Mnapewa crown na mnajua hamjafuzu Yaani chupa ya bia mnabebea maji ya uzu

Kugwehana yamekukuta pole mpwa Umejikula leba kisa majibu ya nectar Akili za watoto siungi mkono Ninyongewe haifai mwanangu nitizame pono

Hii barua sio chafu kwa iyo sina mashaka Ukingoja muunganiko kumido mlevi wa bapa Barua hii sio ya Wakorintho Wala haina uwezo wowote wa kumrudisha Kristo

Ah-ah naomba msiniite mi nabii Ambaye nimeshushwa kwa ukoo wa kizazi hiki Ah-ah mi nimeandika tu barua Na sina maana kama nafaa kuitwa Masii

Kiri Records! 

(Lets take over the game)


Advertisement


You May Also Like

Embassy of Lebanon in New Delhi, India

Advertisement Address: H 1, Anand Niketan, Chanakyapuri City: New Delhi Fax: 011…

Ulefone T2 specification and features

Advertisement Network Technology GSM / CDMA / HSPA / EVDO / LTE…

Pete Davidson Taking A Step Back From Saturday Night Live For Movie Roles

Advertisement Pete Davidson was absent from Saturday Night Live this weak for…

Who are you talking to

Advertisement Who are you talking to meaning? “Talking to” someone means that…